"Create Memories, One Joint @ a Time” “Unleash the Soundtrack to Your Life” “Where Music Meets Magic” “Elevating Vibes, Amplifying Experience with almost every gerne of music. Lets get it.
New Track kutoka kwa Member wa iliyokuwa East Coast Team toka Upanga, King Crazy GK amevunja ukimya kwa kuachia ngoma mpya ambayo amewashirikisha Venessa Mdee, Rawdgers na J-Hoox inayokwenda kwa Jina la Shukrani. Ngoma hii imetoka Juzi baada ya Kimya Kirefu toka kwa Mkongwe huyu na Imefanywa chini ya Uangalizi wa Producer John Mahundi.
Ukitaka kuisikia/Kuipakua Bofya hii link hapa chini.
Mwanamuziki anayewakilisha Mziki wa Kizazi kipya ndani “Dullayo”, amekuja na Ngoma Mpya akimshirikisha Mkongwe “Prof Jay” na Track iliyopewa jina la “Moko moko” Ngoma hii imefanywa katika Studio za Mwanalizombe chini ya Producer Mashuhuri “Villy” Enjoy ngoma hii na Tutoe support kwa wasanii wetu wa Miziki ya aina Zote ndani ya Bongo. Bofya hii link hapo chini Kuisikia na Kuipakua ngoma hii.
Masela wangu, Wana Wote na Wapenzi wa Bongo Hip hop Music, I did a Mix to End This year 2014. Basi hii hapa Non-Stop Mix kwa Decemeber hii tayari kuingia Mwaka Mpya. Merry Christmas and Happy New year to Everybody. Fuata Link hii kusikiliza Mix hii. STAY BLESSED.
Kile kichupa kipya tulichokuwa tukikisubiria kwa Hamu toka kwa General Digiriii aka Jcb ft Ben Pol titled “I don’t care” kimetoka na ndio hiki hapa. Fanya kukicheck na kusambazia wana wote wanao support hip-hop ya Bongo.
“Big 4 the Geez” ukipenda Unaweza Kumuita “Mwanamadharau” ama wengi walimuita “Geez Mabovu Jina kamili “Ahmed Ally Utepe” alikuwa ni Msanii wa Kizazi kipya aliyefanya mziki wa hip hop toka “Dirty South” Iringa, Tanzania. Geez alifariki dunia siku ya Tarehe 12 Mwezi wa 11 Mwaka huu baada ya kuumwa kwa muda mrefu. Wakati wa uhai wake alikuwa ni kati ya wasanii wachache ambao waliitendea haki Hip hop nchini Tanzania.
Haukujalisha Mziki huu ulimlipa kiasi gani katika soko la Muziki wa kizazi kipya nje na ndani ya Bongo, Mchizi aligangamaa na kuendelea kufanya kazi yake ya Sanaa tokana na Mapenzi ya sanaa na kazi yake. Mtoto huyu wa kiume hakuyumbishwa tokana na air-time rediaoni ama kuandikwa mara kwa mara katika blogs ama kutangazwa na vyombo vya habari kwa nia ya kumpatia kipato zaidi, alipiga moyo konde ingawa ilikuwa ni ngumu ila hakufa moyo. Alikuwa na Urafiki wa karibu na wasanii toka Chemba Squad pia wasanii kadhaa toka Arachuga A-town city.
Mimi pia nilikuwa ni shabiki mkubwa wa kazi zake na nilivutiwa zaidi na Style yake ya Kughani pamoja na sauti yake nzito ukilinganisha na umbo lake, pia mashairi yake ambayo yalikuwa ni ya kitaa zaidi yalikuwa yamesheheni aliweza ujumbe ulioeleweka kirahisi pindi ukimtegea sikio. Siku 3 baada ya Kifo chake nilipokea Maombi mengi toka kwa washabiki wake wakiniomba nifanye (Non-Stop) Mix ambayo itaenzi mziki wa GEEZ MABOVU nami sikufanya ajizi. Basi kama wewe ni Mshabiki wake wa kweli na ungependa kuendelea kumkumbuka Fanya kubofya link hii hapa chini usikilize/uipakue Mix hii Bure kama kumbukumbu ya kazi za Geez. #ForTheLoveOfHiphop #GeezMabovuTributeMix #RIPDirtySouthDawg
Mashabiki wote wa Bongo Hip hop, hii ni zawadi mpya toka kwa The GENERAL himself, toka katika Kundi la watengwa. This time amekuja na GHETTO LOVE joint, ambayo itakufanya moyo wako ukusisimuke. JCB ameachia “Mtoto Mkali” leo Rasmi kwa wana wote na wapenzi wa Hip hop baada ya muda kidogo maana yupo mbio na shughuli zake za maisha. Ngoma ni kali, Support Bongo Hip hop kama wewe ni mpenzi wa kweli wa huu mziki. Click link hii kuweza kuusikiliza na kuupakua hapa chini:
Hii hapa ngoma mpya ya YOUNG KILLER akimshirikisha kaka yako toka Rock City Mwanza FID Q. Ngoma hii ina michano ya kweli sana. Kama wewe ni mpenzi wa Bongo Hiphop na unafuatilia kazi za hawa jamaa, fanya kuingia YouTube hapa chini ku-enjoy hili dongo. Naambatanisha mashairi ya huu wimbo baada ya video, Enjoy!
Stream the audio here:
VERSE 1:
Mama ndie alie nitabiri mi nitakua star na nyota wa kila pande/ Nikiwa na raha.. kwa mwenye hasira nisijigambe/
Usimpige mkeo piga shangwe/
Kwa maana Young killer sio ngazi.. kwa hiyo mwambieni shetani asinipande/
I Think big.. its my dream biggie kuwa/
Bigger wa michano nigga ambaye hata Jigga atanijua/
Kuwa msodoki nawaficha mistari/Upeo wangu umekula mchicha na ndo maana nina fikra za kuona mbali/
Msukuma anae sukuma mitikasi ikatulia/
Hata ‘ Francis Cheka ‘ naweza mpiga panchi akalia/
Wanaoijua njaa ndo wanaamini cha kwanza kilimo/
Mi sijagombania ustar ili nikifa nikazikwe kino/
Wabovu wakichana ‘ IMO ‘ na hawazijui nguzo tano/
Leo kwenye ustar ‘ simo ‘ kisa sina muonekano?/
Mi nina POWER.. ya ibada nilioiomba baada ya kipato/
Pole dada ulie nitosa kisa umenizidi kidato/
Futa jasho na damu saka noti ‘hali tete’ /
Watoto wanamjua Diamond na Joti”” zaidi ya Kikwete/
Popote niko fiti…tega skio/
Shoga hata akitoa jicho vipi…hawezi kuyaona mafanikio..ndio
Chorus:
Ni MSODOKI na NGOSHA.. Miujiza iliyotabiriwa haina haja ya kuogopa/ Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi/Lakini ninaweza zitengeneza nikiongeza juhudi/ Tangu Agosti tangu April.. YEAAAH.. tangu Agosti tangu April/ Nina Hustle bila wasi wala hofu/ MUNGU wangu hawezi nipa shida ambayo nitashindwa kuisolve
VERSE 2:
Wakisha amini unawahitaji zaidi ya wanavyokuhitaji/ Mapenzi ya ‘ wadau wa mjini ‘ hugeuka ya ‘ samaki na maji ‘/ Uishi ndani yake tu… nje yake uvuliwe/ Kwa msaada wake upikwe kisha yawanawishe.. uliwe/
SIKUUMBWA nije kusettle for less/ Nitaisubiri mvua inyeshe.. nijitokeze kudance/ Nonsense sitemi/ asset sio deni/ HOMEBOY.. natema vitu on point.. jifunzeni/ THAMINI HUU MUDA kabla haujageuka HISTORY/ Part of the PAST dont fit the script for the FUTURE memory/ Niliyoyapitia… yameniandaa kwa haya yajayo/ Sio dalili ya kusinzia.. ni ‘ NJAA ‘ nikipiga mihayo/ MASKINI.. ninajiamini hadi natokwa na ukungu/ Bila ujuzi wasingenithamini.. NINGETOSWA mpaka na ndugu/ Kitachonizamisha sio kudondoka mtoni/ Ni kushindwa kupiga mbizi na kusizi ili msinione…
Ni MSODOKI na NGOSHA.. Miujiza iliyotabiriwa haina haja ya kuogopa/ Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi/Lakini ninaweza zitengeneza nikiongeza juhudi/ Tangu Agosti tangu April.. YEAAAH.. tangu Agosti tangu April/ Nina Hustle bila wasi wala hofu/ MUNGU wangu hawezi nipa shida ambayo nitashindwa kuisolve
VERSE 3:
FQ- Napenda umaarufu.. ninachukia MBWEMBWE zake/ Au ninapospit truth kwa booth halafu WAKUSHI hamninyaki/ Ninauacha uchi ‘ UKWELI ‘ uzushi sio mwake/ Hata mkigushi mtafeli.. hamnigusi na hamnipati/
YK- Siamini nimekua MIMI hadi hii leo nimefika hapa/ Aliyenilea hakuniamini.. niliyemtegemea hakunitaka/ Bila nyinyi.. WADAU.. Ninakili sishiki sarafu/ Na ndo maana sili bata kwa maana BATA WACHAFU/ Kuwa mkali wa kusifiwa.. kubali kutumiwa/ Nilichoambiwa kuwa ‘ sikuhizi hadi wajanja wanaliwa’/ Inatakiwa kuwa STRIKER..Mambo yaende SCHKOPA/ Kama haujanileta.. hauwezi kunirudisha nilikotoka…
Mdau wa Mziki wa Kizazi kipya ndani ya Bongo na Kwengineko. Pokea kazi mpya toka kwa wakongwe hawa wawili katika kuihamasisha jamii ya ki TANZANIA kuhusu hali ya sasa na Uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015. Wimbo umefanywa Mwanalizombe Records chini ya Producer Villy.
Bofya hii Link hapa Chini Uisikie/Uipakue Bureeeee, Enjoy!
Kwa wale watu wangu tunao support Mziki wa Bongo hasa Bongo Hip hop Check out New Banger toka Kwa MWANAHAPA. Ngoma hii ambayo ni ya Ukweli ina ujumbe mzito katika jamii yetu inaitwa BWANA MDOGO Chini ya Uangalizi wa PRODUCER: SALLII TEKNIKS na Kufanyiwa MIXING na JAY ADEAN Katika Studios za ROCK TOWN RECORD.