Bongo Radio Throwback Monday Show June 2nd 2014 Part 1(C)Ngomanagwa.
Hii ni Show ya Jana yenye Ngoma za Zamani za Afrika Mashariki. Hili ni Saa la Kwanza la Show na Lisaa la Pili nitali-upload Alhamisi hii. Enjoy Good Music and Show, Stay Blessed.
Bongo Radio Throwback Monday Show June 2nd 2014 Part 1(C)Ngomanagwa.
Hii ni Show ya Jana yenye Ngoma za Zamani za Afrika Mashariki. Hili ni Saa la Kwanza la Show na Lisaa la Pili nitali-upload Alhamisi hii. Enjoy Good Music and Show, Stay Blessed.
Oldskool Bongo Finest May 2014 (C)Ngomanagwa.
Hii Hapa ni Mix Fupi yenye ngoma chache ambazo ziliwahi kuvuma na moja mbili adimu. Kwenye hii Mix utasikia wasanii na makundi kama Hard blasters, Kwanza Unit, Deplowmatz, Suma G na Hashim Dogo. Ukipenda Unaweza kuisikiliza na Kuishusha HAPA>>>http://hu.lk/guz6bejj01z4

Tokana na Malalamiko toka kwa wasikilizaji wa Mixes na Wapenzi wa Mziki wa Bongo kuwa nabagua kufanya Mixes za Miziki mingine na Kufanya Bongo Hip hop Mixes peke yake ama Sana. Nimesikia Kilio chenu na Nawaletea NEW Mix ya “BONGO FLAVA” kwa Mwezi “MAY” Mwaka 2014 kwa ajili yenu. Nyimbo zote humu ni Mpya. Enjoy
Bongo Radio Throwback Monday Show May 12th 2014 (C)Ngomanagwa.

Kama Ungependa kuisikiliza ama Kuidownload Show Ingia hapa>>>http://hu.lk/7yn80h1fk2kg

Hawa ni Vijana Kutoka Kinondoni wanaokwenda kwa Jina la Big Dogg Posse. Kundi hili liliundwa Mwaka 1994 na lilikuwa na Jumla wa wasanii watatu waliokuwa wakiwakilisha. Majina ya wasanii hao ni KOMPYUTAH, DRAYZI CHIEF and CHRONIC FINGER. Mwaka 2000 walitoka na Single yao matata ambayo ilikuwa ni Bonge la Hit katika maredio na Matamasha iliyokwenda kwa jina la “Rudi Mpenzi” waliyoifanya katika Studio za MJ pale Oysterbay. Pia walitoa Ngoma nyingine kama “Wosia” pamoja na “Bahati ya Mwenzio” ambazo zilikuwemo katika album yao ya Kwanza.
Kutokana na Kufanya Vizuri katika Soko la Muziki wa Kizazi Kipya Vijana hawa wa Kinondoni Waliingia Studio Kufanya Santuri ya Pili iliyokwenda kwa Jina la “BDP KAMILI”. Santuri hii ilibeba Ngoma kama “Ma jobless” ambayo ndio ilikuwa Single yao ya kwanza ambayo ilifuatiwa na “Kumwambia” na nyinginezo kibwena. Kwa Kifupi walitikisa sana Jiji la Dar na Vitongoji vyake mara walipopanda kwenye Majukwaaa ya Matamasha na Walikuwa na wapenzi wengi sana. Mziki wao ulikubalika sana ndani ya Bongo. Bofya hapa Kusikiliza Ngoma zao Mbili toka katika Santuri yao ya Kwanza.
