"Create Memories, One Joint @ a Time” “Unleash the Soundtrack to Your Life” “Where Music Meets Magic” “Elevating Vibes, Amplifying Experience with almost every gerne of music. Lets get it.
Mashabiki wote wa Bongo Hip hop, hii ni zawadi mpya toka kwa The GENERAL himself, toka katika Kundi la watengwa. This time amekuja na GHETTO LOVE joint, ambayo itakufanya moyo wako ukusisimuke. JCB ameachia “Mtoto Mkali” leo Rasmi kwa wana wote na wapenzi wa Hip hop baada ya muda kidogo maana yupo mbio na shughuli zake za maisha. Ngoma ni kali, Support Bongo Hip hop kama wewe ni mpenzi wa kweli wa huu mziki. Click link hii kuweza kuusikiliza na kuupakua hapa chini:
Hii hapa ngoma mpya ya YOUNG KILLER akimshirikisha kaka yako toka Rock City Mwanza FID Q. Ngoma hii ina michano ya kweli sana. Kama wewe ni mpenzi wa Bongo Hiphop na unafuatilia kazi za hawa jamaa, fanya kuingia YouTube hapa chini ku-enjoy hili dongo. Naambatanisha mashairi ya huu wimbo baada ya video, Enjoy!
Stream the audio here:
VERSE 1:
Mama ndie alie nitabiri mi nitakua star na nyota wa kila pande/ Nikiwa na raha.. kwa mwenye hasira nisijigambe/
Usimpige mkeo piga shangwe/
Kwa maana Young killer sio ngazi.. kwa hiyo mwambieni shetani asinipande/
I Think big.. its my dream biggie kuwa/
Bigger wa michano nigga ambaye hata Jigga atanijua/
Kuwa msodoki nawaficha mistari/Upeo wangu umekula mchicha na ndo maana nina fikra za kuona mbali/
Msukuma anae sukuma mitikasi ikatulia/
Hata ‘ Francis Cheka ‘ naweza mpiga panchi akalia/
Wanaoijua njaa ndo wanaamini cha kwanza kilimo/
Mi sijagombania ustar ili nikifa nikazikwe kino/
Wabovu wakichana ‘ IMO ‘ na hawazijui nguzo tano/
Leo kwenye ustar ‘ simo ‘ kisa sina muonekano?/
Mi nina POWER.. ya ibada nilioiomba baada ya kipato/
Pole dada ulie nitosa kisa umenizidi kidato/
Futa jasho na damu saka noti ‘hali tete’ /
Watoto wanamjua Diamond na Joti”” zaidi ya Kikwete/
Popote niko fiti…tega skio/
Shoga hata akitoa jicho vipi…hawezi kuyaona mafanikio..ndio
Chorus:
Ni MSODOKI na NGOSHA.. Miujiza iliyotabiriwa haina haja ya kuogopa/ Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi/Lakini ninaweza zitengeneza nikiongeza juhudi/ Tangu Agosti tangu April.. YEAAAH.. tangu Agosti tangu April/ Nina Hustle bila wasi wala hofu/ MUNGU wangu hawezi nipa shida ambayo nitashindwa kuisolve
VERSE 2:
Wakisha amini unawahitaji zaidi ya wanavyokuhitaji/ Mapenzi ya ‘ wadau wa mjini ‘ hugeuka ya ‘ samaki na maji ‘/ Uishi ndani yake tu… nje yake uvuliwe/ Kwa msaada wake upikwe kisha yawanawishe.. uliwe/
SIKUUMBWA nije kusettle for less/ Nitaisubiri mvua inyeshe.. nijitokeze kudance/ Nonsense sitemi/ asset sio deni/ HOMEBOY.. natema vitu on point.. jifunzeni/ THAMINI HUU MUDA kabla haujageuka HISTORY/ Part of the PAST dont fit the script for the FUTURE memory/ Niliyoyapitia… yameniandaa kwa haya yajayo/ Sio dalili ya kusinzia.. ni ‘ NJAA ‘ nikipiga mihayo/ MASKINI.. ninajiamini hadi natokwa na ukungu/ Bila ujuzi wasingenithamini.. NINGETOSWA mpaka na ndugu/ Kitachonizamisha sio kudondoka mtoni/ Ni kushindwa kupiga mbizi na kusizi ili msinione…
Ni MSODOKI na NGOSHA.. Miujiza iliyotabiriwa haina haja ya kuogopa/ Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi/Lakini ninaweza zitengeneza nikiongeza juhudi/ Tangu Agosti tangu April.. YEAAAH.. tangu Agosti tangu April/ Nina Hustle bila wasi wala hofu/ MUNGU wangu hawezi nipa shida ambayo nitashindwa kuisolve
VERSE 3:
FQ- Napenda umaarufu.. ninachukia MBWEMBWE zake/ Au ninapospit truth kwa booth halafu WAKUSHI hamninyaki/ Ninauacha uchi ‘ UKWELI ‘ uzushi sio mwake/ Hata mkigushi mtafeli.. hamnigusi na hamnipati/
YK- Siamini nimekua MIMI hadi hii leo nimefika hapa/ Aliyenilea hakuniamini.. niliyemtegemea hakunitaka/ Bila nyinyi.. WADAU.. Ninakili sishiki sarafu/ Na ndo maana sili bata kwa maana BATA WACHAFU/ Kuwa mkali wa kusifiwa.. kubali kutumiwa/ Nilichoambiwa kuwa ‘ sikuhizi hadi wajanja wanaliwa’/ Inatakiwa kuwa STRIKER..Mambo yaende SCHKOPA/ Kama haujanileta.. hauwezi kunirudisha nilikotoka…
Kwa wale watu wangu tunao support Mziki wa Bongo hasa Bongo Hip hop Check out New Banger toka Kwa MWANAHAPA. Ngoma hii ambayo ni ya Ukweli ina ujumbe mzito katika jamii yetu inaitwa BWANA MDOGO Chini ya Uangalizi wa PRODUCER: SALLII TEKNIKS na Kufanyiwa MIXING na JAY ADEAN Katika Studios za ROCK TOWN RECORD.
New Mix with a lot of Xclusive Bangerz from Tanzanian Hip hop Scene. In this Mix you can here Hip hop Artists like Fid Q, Prof Jay, Songa, Nikki Mbishi, P the Emcee, Juma Nature, Panishit, Stamina, B.O.B Micharazo etc, Enjoy.
For all those who like Throwback Music and Missed my LIVE Show on BONGO RADIO, here it is. Enjoy 2 hrs with Throwback Music From East Africa, Lets get it.
For individuals who have a deep appreciation for quality hip hop music, particularly the boom bap style, you have arrived at the perfect destination. The mix titled “Bongo Hip Hop Mix June 2014,” curated by DJ Ngomanagwa, was uploaded a decade ago. I have chosen to re-upload it due to the previous link becoming inactive. Immerse yourself in the vibrant sounds of Tanzanian hip hop and please remember to share your thoughts in the comments section.
Hii ni Show ya Jana yenye Ngoma za Zamani za Afrika Mashariki. Hili ni Saa la Kwanza la Show na Lisaa la Pili nitali-upload Alhamisi hii. Enjoy Good Music and Show, Stay Blessed.
Hii Hapa ni Mix Fupi yenye ngoma chache ambazo ziliwahi kuvuma na moja mbili adimu. Kwenye hii Mix utasikia wasanii na makundi kama Hard blasters, Kwanza Unit, Deplowmatz, Suma G na Hashim Dogo. Ukipenda Unaweza kuisikiliza na Kuishusha HAPA>>>http://hu.lk/guz6bejj01z4
Tokana na Malalamiko toka kwa wasikilizaji wa Mixes na Wapenzi wa Mziki wa Bongo kuwa nabagua kufanya Mixes za Miziki mingine na Kufanya Bongo Hip hop Mixes peke yake ama Sana. Nimesikia Kilio chenu na Nawaletea NEW Mix ya “BONGO FLAVA” kwa Mwezi “MAY” Mwaka 2014 kwa ajili yenu. Nyimbo zote humu ni Mpya. Enjoy