Category: News

All news about music artist and upcoming work.

(Audio) Big Dogg Posse “BDP Kamili”

BDP
Hawa ni Vijana Kutoka Kinondoni wanaokwenda kwa Jina la Big Dogg Posse. Kundi hili liliundwa Mwaka 1994 na lilikuwa na Jumla wa wasanii watatu waliokuwa wakiwakilisha. Majina ya wasanii hao ni KOMPYUTAH, DRAYZI CHIEF and CHRONIC FINGER. Mwaka 2000 walitoka na Single yao matata ambayo ilikuwa ni Bonge la Hit katika maredio na Matamasha iliyokwenda kwa jina la “Rudi Mpenzi” waliyoifanya katika Studio za MJ pale Oysterbay. Pia walitoa Ngoma nyingine kama “Wosia” pamoja na “Bahati ya Mwenzio” ambazo zilikuwemo katika album yao ya Kwanza.

Kutokana na Kufanya Vizuri katika Soko la Muziki wa Kizazi Kipya Vijana hawa wa Kinondoni Waliingia Studio Kufanya Santuri ya Pili iliyokwenda kwa Jina la “BDP KAMILI”. Santuri hii ilibeba Ngoma kama “Ma jobless” ambayo ndio ilikuwa Single yao ya kwanza ambayo ilifuatiwa na “Kumwambia” na nyinginezo kibwena. Kwa Kifupi walitikisa sana Jiji la Dar na Vitongoji vyake mara walipopanda kwenye Majukwaaa ya Matamasha na Walikuwa na wapenzi wengi sana. Mziki wao ulikubalika sana ndani ya Bongo. Bofya hapa Kusikiliza Ngoma zao Mbili toka katika Santuri yao ya Kwanza.