Category: News

All news about music artist and upcoming work.

(Audio) Tha De-Plow-Ma-TZ

dpt-99
De-Plow-Matz
Members: Dola, Saigon, Stigo, Trip Dogg
Albums: Are you down with the DPT (96), Tha De-Plow-MaTZ (97)

Katikati ya Miaka ya 90’s, Saigon na Stigo waliungana na Dola Soul ambaye alikuwa ndio amerudi toka Lagos nchini Nigeria alipokulia. Walianza Kurekodi Ngoma chache katika Studio na P- Funk na Master Jay na Matokeo yake ilikuwa ni Santuri ya De-Plow-Matz. Style zao za Ku-Flow zilikuwa ni mpya katika masikio wa wapenzi wa Mziki wa kizazi kipya nchini Tanzania. Ngoma walizowahi Kuzitoa kama Kundi ni kama, ” Turuke kwa Furaha, Are You down, Tanzania” pia Solo Track ya Saigon iliyoitwa, ” Take a ride” ambazo zilikuwa maarufu sana katika vituo vya Redio na TV.

Mnamo Mwaka 1999 Members wote wa De-Plow-Matz walikuwa wameondoka Bongo Kuelekea Ughaibuni kwa Masomo akiwemo Saigon, Trip Dogg pamoja na Stigo na Kumuacha Dola Soul Peke Yake akiendelea Kuipeperusha Bendera Ya Kundi. Hapo Jamaa akaamua kufanya Solo Album ambayo ilipata Mafanikio Sana ndani ya Bongo ambayo ilikuwa na Ngoma Kama, “Nani na nani, Kwenye Chati n.k” Sasa Hivi Dola Yupo Chicago akiishi na Familia yake, Saigon alirudi Bongo na anaendelea kufanya mziki, Stiggo Yupo New York akiishi pamoja na Ku Produce Mziki katika Studio za S&S na Trip dogg yupo UK. Kwa Historia hii fupi ya kundi hili, Sikiliza Ngoma zao tatu hapa ikiwemo Track Moja ambayo Dola Alifanya kama Solo Artist. Bofya hizi Links kuweza kusikiliza hizi Nyimbo.

(Audio) 2Proud – Ni Wapi? (Throwback Joint of the Day)

2Proud
Ni wapi tunakwenda, tu-tu-tunakwenda,… hivyo ndivyo kiitikio cha huu wimbo kinavyosikika. Track hii ilikuwa maarufu sana ilipotoka mwaka 95′.

Ni moja kati ya Nyimbo kali ambazo zilishawahi toka miaka ya 90’s Tanzania. Album ambayo ilibeba ngoma hii na nyingine Kibao ambazo zilikuwa na Mafunzo katika jamii yetu ilipewa Jina la Ni Mimi 1995 Msannii huyu. Mkali wa Miondoko ya Rap za Bongo ambae ni Mkongwe katika game, ambae alitumia majina lukuki katika safari yake ya Muziki kama 2Proud ama Mr II ama Sugu ama Ukipenda Unaweza Kumuita kwa Jina Halisi Joseph Mbilinyi ambaye Pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ana Albums Kumi ambazo ni nyingi kuliko msanii yoyote yule wa muziki wa kizazi kipya aliyewahi Kufanya hivyo Tanzania.

Majina Ya album hizo ni Ni Mimi ya 1995,Ndani ya Bongo 1996, Niite Mister II ya 1998, Nje ya Bongo ya 1999, Millenium ya 2000, Muziki na Maisha ya 2001, Itikadi ya 2002, Sugu ya 2004, Ujio wa Umri ya 2006, Pamoja na VETO ya 2009.Hio ni Historia Fupi tuu kumhusu yeye. EnJoy!

Kubofya Hapa:

(Audio) Unique Sistaz Featuring Hashim Dogo – Sikiliza

Ukipenda unaweza kuwaita Unique Dadaz, katika Ngoma hii ambayo ni ya mwaka 1999 ukiachia mbali nyimbo kama Leo ni Leo na Hot Summer day ambazo waliwahi kuzitoa kabla ya hii na kuwavutia sana mashabiki wao hasa Vijana. Majina yao ni Radhia na Rahima na ni watoto wa Ahmed na Sango Kipozi. Pia wameshawahi kufanya kazi na wasanii wengine wengi akiwemo Mac D. Enjoy

#OldskoolJointOfTheDay.

Bofya hapa kusikiliza huu wimbo hapa: