(Audio) 2Proud – Ni Wapi? (Throwback Joint of the Day)

2Proud
Ni wapi tunakwenda, tu-tu-tunakwenda,… hivyo ndivyo kiitikio cha huu wimbo kinavyosikika. Track hii ilikuwa maarufu sana ilipotoka mwaka 95′.

Ni moja kati ya Nyimbo kali ambazo zilishawahi toka miaka ya 90’s Tanzania. Album ambayo ilibeba ngoma hii na nyingine Kibao ambazo zilikuwa na Mafunzo katika jamii yetu ilipewa Jina la Ni Mimi 1995 Msannii huyu. Mkali wa Miondoko ya Rap za Bongo ambae ni Mkongwe katika game, ambae alitumia majina lukuki katika safari yake ya Muziki kama 2Proud ama Mr II ama Sugu ama Ukipenda Unaweza Kumuita kwa Jina Halisi Joseph Mbilinyi ambaye Pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ana Albums Kumi ambazo ni nyingi kuliko msanii yoyote yule wa muziki wa kizazi kipya aliyewahi Kufanya hivyo Tanzania.

Majina Ya album hizo ni Ni Mimi ya 1995,Ndani ya Bongo 1996, Niite Mister II ya 1998, Nje ya Bongo ya 1999, Millenium ya 2000, Muziki na Maisha ya 2001, Itikadi ya 2002, Sugu ya 2004, Ujio wa Umri ya 2006, Pamoja na VETO ya 2009.Hio ni Historia Fupi tuu kumhusu yeye. EnJoy!

Kubofya Hapa:

Leave a comment