DJ Mix | Geez Mabovu Tribute Mix Nov 2014 ©️ DJ NGOMANAGWA

Geez Mabovu Tribute Mix

“Big 4 the Geez” ukipenda Unaweza Kumuita “Mwanamadharau” ama wengi walimuita “Geez Mabovu Jina kamili “Ahmed Ally Utepe” alikuwa ni Msanii wa Kizazi kipya aliyefanya mziki wa hip hop toka “Dirty South” Iringa, Tanzania. Geez alifariki dunia siku ya Tarehe 12 Mwezi wa 11 Mwaka huu baada ya kuumwa kwa muda mrefu. Wakati wa uhai wake alikuwa ni kati ya wasanii wachache ambao waliitendea haki Hip hop nchini Tanzania.

Haukujalisha Mziki huu ulimlipa kiasi gani katika soko la Muziki wa kizazi kipya nje na ndani ya Bongo, Mchizi aligangamaa na kuendelea kufanya kazi yake ya Sanaa tokana na Mapenzi ya sanaa na kazi yake. Mtoto huyu wa kiume hakuyumbishwa tokana na air-time rediaoni ama kuandikwa mara kwa mara katika blogs ama kutangazwa na vyombo vya habari kwa nia ya kumpatia kipato zaidi, alipiga moyo konde ingawa ilikuwa ni ngumu ila hakufa moyo. Alikuwa na Urafiki wa karibu na wasanii toka Chemba Squad pia wasanii kadhaa toka Arachuga A-town city.

Mimi pia nilikuwa ni shabiki mkubwa wa kazi zake na nilivutiwa zaidi na Style yake ya Kughani pamoja na sauti yake nzito ukilinganisha na umbo lake, pia mashairi yake ambayo yalikuwa ni ya kitaa zaidi yalikuwa yamesheheni aliweza ujumbe ulioeleweka kirahisi pindi ukimtegea sikio. Siku 3 baada ya Kifo chake nilipokea Maombi mengi toka kwa washabiki wake wakiniomba nifanye (Non-Stop) Mix ambayo itaenzi mziki wa GEEZ MABOVU nami sikufanya ajizi. Basi kama wewe ni Mshabiki wake wa kweli na ungependa kuendelea kumkumbuka Fanya kubofya link hii hapa chini usikilize/uipakue Mix hii Bure kama kumbukumbu ya kazi za Geez. #ForTheLoveOfHiphop #GeezMabovuTributeMix #RIPDirtySouthDawg

Leave a comment