(Audio) Tha De-Plow-Ma-TZ

dpt-99
De-Plow-Matz
Members: Dola, Saigon, Stigo, Trip Dogg
Albums: Are you down with the DPT (96), Tha De-Plow-MaTZ (97)

Katikati ya Miaka ya 90’s, Saigon na Stigo waliungana na Dola Soul ambaye alikuwa ndio amerudi toka Lagos nchini Nigeria alipokulia. Walianza Kurekodi Ngoma chache katika Studio na P- Funk na Master Jay na Matokeo yake ilikuwa ni Santuri ya De-Plow-Matz. Style zao za Ku-Flow zilikuwa ni mpya katika masikio wa wapenzi wa Mziki wa kizazi kipya nchini Tanzania. Ngoma walizowahi Kuzitoa kama Kundi ni kama, ” Turuke kwa Furaha, Are You down, Tanzania” pia Solo Track ya Saigon iliyoitwa, ” Take a ride” ambazo zilikuwa maarufu sana katika vituo vya Redio na TV.

Mnamo Mwaka 1999 Members wote wa De-Plow-Matz walikuwa wameondoka Bongo Kuelekea Ughaibuni kwa Masomo akiwemo Saigon, Trip Dogg pamoja na Stigo na Kumuacha Dola Soul Peke Yake akiendelea Kuipeperusha Bendera Ya Kundi. Hapo Jamaa akaamua kufanya Solo Album ambayo ilipata Mafanikio Sana ndani ya Bongo ambayo ilikuwa na Ngoma Kama, “Nani na nani, Kwenye Chati n.k” Sasa Hivi Dola Yupo Chicago akiishi na Familia yake, Saigon alirudi Bongo na anaendelea kufanya mziki, Stiggo Yupo New York akiishi pamoja na Ku Produce Mziki katika Studio za S&S na Trip dogg yupo UK. Kwa Historia hii fupi ya kundi hili, Sikiliza Ngoma zao tatu hapa ikiwemo Track Moja ambayo Dola Alifanya kama Solo Artist. Bofya hizi Links kuweza kusikiliza hizi Nyimbo.

One thought on “(Audio) Tha De-Plow-Ma-TZ

  1. Andiko zuri sana, ila inatia kiu zaidi kutaka kujua na kuzisikia nyimbo zao nyingine na zipatikane online, sanaa yetu haina maktaba, hakuna hifadhi ya taarifa muhimu kama hizi.

    Liked by 1 person

Leave a reply to Mohamed Abdul Cancel reply